April 27, 2008

Leo pata shika katika Ligi ya Ujerumani

Luca Toni na Gomez

wakati mabingwa watetezi wa ujerumani Stuttgart wanapokuta na mabingwa watarajiwa Bayern Munich. Macho ya mashabiki wa ujerumani yatakodolewa Leo katika mpambano wa kukata na shoka baina ya mabingwa Stuttgart na viongozi wa Bundesliga-Bayern Munich.Munich imefungua mwanya wa hadi pointi 10 kutoka Schalke na ingawa ilishimndwa juzi kutamba katika nusu-finali ya kombe la ulaya la UEFA huko Petersburg,Russia, inahitaji pointi zote 3 kesho kumaliza udhia na kutia mfukoni kombe lake la pili msimu huu.Wiki iliopita, Munich ilitoa B.Dortmund kwa mabao 2:1 na kutawazwa mabingwa wa kombe la shirikisho la kabumbu la Ujerumani DFB.Munich imepania kutwaa vikombe 3 msimu huu.

No comments: