May 22, 2008

ALI KIBA kukamua Miss Tanzania EU 08‏

"Cinderella"," Nakshi nakshi" na Miss Schengen 08 ndani ya Germany 28.06.08, Essen .. Katika shindano la kumsaka mrembo wa Schengen 2008 , burudani itatolewa na msanii Ali Kiba ambaye ameahidi kurusha nyoyo za wapenzi wake usiku huo wa raha. Katika sakata hilo Mgeni rasmi atakua ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Balozi A.R. Ngemera , Wageni wengine maalum ni mkuu wa Kitengo cha kiswahili radio Deutsche Welle bi Andrea Schimdt, Mratibu wa Beautiful tanzania Agency bi Irene Kiwia na Miss World Africa Nancy Sumari. Akifafanua zaidi Mratibu wa Shindano la Miss Tanzania Schengen bi Nashe Mvungi ameelezea kuwa kwa mara ya kwanza Miss Tanzania kushirikisha mrembo kutoka Schengen 2008, Ambapo mwaka jana UK ilikuwa ya kwanza kushirikisha mrembo kutoka nje ya bara la Afrika .Nia ni kutaka kupanua utamaduni na mila ya mtanzania ulimwenguni, kushirikisha watanzania walio masomoni au wanaoishi ughaibuni katika kuchangia maendeleo ya tanzania kiutalii na elimu na kuweka uhusinao katika ya jamii iliyoko nyumbani na Ulaya.Pia alipenda kufafanua kuwa shindano hili limepitishwa na kupewa baraka zote na Uncle Hashim Lundenga wa LINO International agency waandaaji wa miss Tanzania.Mshindi wa shindano hili atajipatia zawadi ya ticket na nafasi ya kushiriki shindano la kitaifa August 2008 Dar es salaam.
info@misstanzania.eu
Tel.+49 1520 588 0863

No comments: