Mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 16 anaendelea kupata matibabu hospitalini baada ya kupoteza sehemu ya uume wake katika tararibu za kutahiriwa nchini Kenya.
Ajali hiyo ilimkumba mtoto huyo wakati kisu alichokuwa akitumia ngariba anayefanya zoezi hilo kumteleza katika sherehe za kutahiriwa za watu wa Luhya waishio magharibi mwa Kenya.
Kufanya tohara kwa njia za kijadi hukosolewa mara nyingi kutokana na athari za kiafya zinazoweza kumkumba anayetahiriwa lakini ni mila ya Kiluyha iliyodumu kwa miaka mingi.
Madakatari wa hospitali hiyo wamesema mtoto huyo anaendelea vizuri lakini huenda akahitaji kufanyiwa upasuaji ili kurudisha upya kiungo hicho.
`Sitomfungulia mashitaka`
Maafisa wa tiba katika hospitali ya wilaya ya Bungoma wameiambia BBC kwamba sehemu ya mwisho ya uume wake ulikatwa kwa bahati mbaya wakati kisu alichokuwa akitumia ngariba huyo kuteleza.
Mtoto huyo amekuwa akifanyiwa upasuaji kuzuia damu kutoka katika uume wake.
Wamesema kuwa ataweza kufanya haja ndogo lakini hatoweza kufanya mapenzi katika siku sa usoni.
Waandishi waliopo huko wamesema upasuaji wa kurudisha upya kiungo hicho kwa mtoto huyo ni gharama kubwa na itamlazimu kwenda nchi za nje kwa upasuaji.
Baba wa mtoto huyo amesema ni ajali iliyotokea bahati mbaya na hana mpango wowote wa kudai fidia wala kumshitaki ngariba huyo.
ataweza kufanya haja ndogo lakini hatoweza kufanya mapenzi katika siku sa usoni.
No comments:
Post a Comment