MANENO MACHAFU NA KASHFA HAZINA NAFASI KATIKA KIWANJA HIKI. TUNAKARIBISHA MAONI YENYE KUJENGA NA KUELIMISHA JAMII.
September 28, 2008
MLIMA KILIMANJARO WALETA MZOZO
Mlima Kilimanjaro umesababisha mzozo miongoni mwa Watanzania na Wakenya wanaoshiriki mafunzo ya utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa, mjini Milwaukee. Tukio hilo lilitokea juzi Septemba mwaka huu, wakati wakiwa darasani katika Chuo Kikuu cha Marquette, mjini hapa, chanzo kikiwa ni Dk. Thomas Bausch, raia wa Marekani, aliposema ni katika miaka ya karibuni amefahamu mlima huo uko Tanzania na si Kenya. "Wamarekani wengi ndivyo wanavyojua, nilishangaa sana," alisema Dk. Bausch na kuongeza kuwa Watanzania wanatakiwa kuutangaza Mlima Kilimanjaro ujulikane uko kwao. Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya Watanzania wanaohudhuria mafunzo hayo ya wiki sita kujibu kwa msisitizo, kwamba Mlima Kilimanjaro uko Tanzania, huku wakimwambia Dk. Bausch, 'karibu Tanzania upande Mlima Kilimanjaro'. Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela ndiye aliyeongoza 'mashambulizi' kwa upande wa Watanzania, kwa kumwambia Dk. Bausch ambaye ni mtu mzima wa makamo kuwa, yeye ni mmoja wa wabunge katika mkoa wa Kilimanjaro na ndiko mlima ulipo. Baadhi ya Wakenya walikuwa wakiingilia kati wakati Anne alipokuwa akimweleza Dk. Bausch kwa kusema 'hata ukiwa Kenya unauona Mlima Kilimanjaro.' Anne aliwataka wanyamaze na kuwaambia kwamba kwa muda mrefu wamekuwa wakieneza uongo huo. "Huo ni uongo wa kimataifa, Mlima Kilimanjaro uko Tanzania," alisisitiza Anne na kuongeza "Katika masuala ya msingi yanayohusu nchi yangu sitaki mchezo." Anne alitoa mfano kwamba, kama mtu ana nyumba yake, na jirani yake anaiona, je jirani huyo anaweza kutangaza ni yake kwa sababu anaiona akiwa kwake?. Dk. Bausch akajibu hapana. Mfanyakazi wa Wizara ya Afya ya Kenya, Sylivia Shitsama, alitoa doa zaidi pale alipohoji, kama hiyo nyumba ina manufaa na haitumiwi, kuna ubaya gani kwa mtu mwingine kuitumia. Kauli hiyo ilifuatiwa na mguno wa nguvu kutoka kwa Watanzania, wakiashiria kutokubaliana naye. Katika hatua nyingine, Dk. Bausch ambaye aliwahi kuwa mshauri wa wanafunzi katika chuo kikuu hicho kwa miaka zaidi ya 10, alisema aliwahi kuzitembelea Tanzania na Kenya. Alisifu Kenya wana chai nzuri, na Anne alimjibu kwamba siku nyingine akirudi Tanzania asikose kuulizia chai ya Njombe kwani nayo ni 'bomba'. Watanzania wengine wanaohudhuria mafunzo hayo, ni Naibu Spika Anne Makinda, Mbunge Injinia Mohamed Mnyaa na Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Caesar Waitara. Wengine ni Hakimu Mkazi Batista Mhelela kutoka mkoa wa Ruvuma, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya afya mkoani Kilimanjaro, Veronica Shao, Mwenyekiti wa Mahakama ya Ardhi na Nyumba mkoa wa Ilala, Dar es Salaam, Lusungu Hongoli na mfanyakazi wa Bunge, Anselm Mrema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22
-
NDUGU,JAMAA, MARAFIKI NA WADAU WA BLOG HII YA JAMII NASIKITIKA KUWATAARIFU YA KUWA NIMEPATWA NA MSIBA WA MAMA YETU MPENDWA BI KHADIJA( NA...
-
blog hii bado inatengenezwa na unakaribishwa kwa maoni. Pia unakaribishwa kuangalia website yetu mpya http://kilimanjarostars.de/ .
No comments:
Post a Comment