Polisi ya Ujerumani imewakamata washukiwa wawili kutoka ndani ya ndege ya abiria ya shirika la ndege la KLM muda mfupi kabla ndege hiyo haijaanza safari yake kuelekea Amsterdam Uholanzi kutoka katika uwanja wa Cologne hapa Ujerumani. Washukiwa hao wawili,kwa mujibu wa polisi ni Msomali mmoja mwenye umri wa miaka 23 na mwingine akiwa raia wa Ujerumani mwenye asili ya Kisomali akiwa na umri wa miaka 24 aliezaliwa Mogadishu.Hata hivyo majina yao hayakutajwa. Msemaji wa idara ya upelelezi katika jimbo la North-Rhine Westfalia kunakopatikana uwanja huo wa ndege ,mbali na kukiri tukio hilo lakini amekanusha madai ya awali kuwa polisi waliivamia ndege hiyo na baadae kukatokea vurumai. Aidha Polisi imesema kuwa wanausalama wamekuwa wakichunguza mienendo ya wanaume hao kwa muda. Pia,polisi ilipofanya upekuzi katika nyumba walimokuwa wakikaa wamekuta kijibarua ambapo watu hao walionyesha nia yao ya kuwa wako tayari kufa katika vita vitakatifu. Ndege hiyo iliruhusiwa baade kuendelea na safari yake hadi Uholanzi ambako inaarifiwa ilifika salama salimini. Na huko nchini Uholanzi kwenyewe mkuu wa idara ya serikali inayopambana dhidi ya ugaidi, anasema kuwa nchi hiyo baado inakabiliwa na tisho la kushambiliwa na makundi ya kigaidi ya kislamu. Hii inatokana na mgogoro wa filamu moja iliotengenezwa na mbunge ambayo inachukuliwa kama inadhalilisha uislamu. Idara ya kitaifa inayoratibu harakati za kupambana dhidi ya ugaidi,katika ripoti yake iliotolewa mapema mwezi huu,ilisema kuwa ile filamu inaitwa FITNA imelifanya taifa hilo kama shabaha ya ugaidi. Haijulikani ikiwa kukamatwa kwa wanaume wawili katika uwanja wa ndege wa Cologne unauhusiano na hilo,ila kukamatwa huko kumekuja siku moja tu baada ya polisi kupata msaada wa wananchi kujaribu kutoa habari za wapi waliko waislamu wawili wenye msimamo mkali.Polisi ilisema kuwa mmoja wa waislamu hao alikuwa raia wa Ujerumani ambae alisilimu. Watu hao wawili wanashukiwa kuwa wanachama wa kundi la kigaidi linalojiita,Islamic Jihad Union, ambalo kawaida linaelezewa kama linalorithi kundi la al-Qaida. Polisi inasema kuwa wanafuatilia alama karibu 20 zinazowahusu Eric Breininger,Mjerumani mwenye umri wa miaka 21 pamoja na Houssain al-Malla Mlebanoni mwenye umri wa miaka 23 ambao walionekana mara ya mwisho katika maeneo yanayoinamia mpaka wa Pakistan na Afghanistan.Polisi inashuku kuwa huenda walirejea Ujerumani kisiri. Polisi inasema kuwa Breininger,anaetoka katika mkoa wa Saarland unaopatikana magharibi mwa Ujerumani, alirekodi mkanda wa Video ambapo alitamka kuwa atafanya shambulio la kujitoa mhanga na kuwa pia eti anaunga mkono jihadi au vita vitakatifu.
MANENO MACHAFU NA KASHFA HAZINA NAFASI KATIKA KIWANJA HIKI. TUNAKARIBISHA MAONI YENYE KUJENGA NA KUELIMISHA JAMII.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22
-
NDUGU,JAMAA, MARAFIKI NA WADAU WA BLOG HII YA JAMII NASIKITIKA KUWATAARIFU YA KUWA NIMEPATWA NA MSIBA WA MAMA YETU MPENDWA BI KHADIJA( NA...
-
blog hii bado inatengenezwa na unakaribishwa kwa maoni. Pia unakaribishwa kuangalia website yetu mpya http://kilimanjarostars.de/ .
No comments:
Post a Comment