Rais Mteule wa Marekani Barack Obama anasubiriwa kutangaza bodi ya wataalam wa uchumi watakaokuwa na jukumu la kumshauri hususan katika masuala ya kuunda nafasi za kazi vilevile kusawazisha mfumo wa fedha unaoyumbayumba.Bwana Obama anatarajiwa kutangaza kundi hilo la wataalam wakati wowote hii leo atakapofanya mkutano wake wa tatu na waandishi wa habari tangu kuchukua wadhifa huo.Kiongozi huyo ameahidi kufanya mabadiliko ya kiuchumi huku msukosuko wa fedha ukiendelea kote ulimwenguni.
Hata hivyo rais huyo mteule alisisitiza umuhimu wa kufuta matumizi yasiyohitajika
Hapo jana Barack Obama alimpendekeza Peter Orszag aliye msimamizi wa kitengo cha bajeti bungeni kuwania nafasi ya msimamizi wa Bajeti katika Ikulu ya Whitehouse.
2 comments:
Kaka umekuwa mwanasiasa wa kimarekani? mbona umeishiwa tupe mada ya taifa letu na matukio muhimu ya jamii yetu ya hapa ulaya na nyumbani kwa ujumla, kama huna funga blog hii usituyeyushe na magazeti yako ya kubuni.
Akhsante Mdau kwa maoni yako madhumuni ya blog hii ni kutoa habari za dunia nzima
akhsante na karibu tena
Malumbo
Post a Comment