December 19, 2008

Gereza la Guantanamo kuwa historia karibuni


Robert Gates.

Wakati serikali mpya ya Marekani itakapoingia madarakani itahakikisha kuwa gereza la Guantanamo litakuwa historia kama anavyosema waziri wa sasa na wa baadaye wa ulinzi nchini humo Robert Gates.Kufuatia   mabadiliko  ya  serikali   nchini  Marekani waziri  wa  ulinzi  wa  nchi  hiyo  Robert  Gates , ambaye  atakuwa  anaendelea  na  wadhifa  huo katika  wizara  hiyo  wakati rais  mteule  Barack Obama  atakapoingia  madarakani ,  amewataka maafisa  wake  kutayarisha  mpango  wa kulifunga  gereza  la  Guantanamo  nchini  Cuba. Mashirika  ya  kutetea  haki  za  binadamu yamekuwa  yakidai   mara  kwa  mara  miaka  kadha iliyopita  kufungwa  kwa  gereza  hilo, ambalo limekuwa  likiwahifadhi  watuhumiwa  tangu  pale baada  ya  shambulio  la  kigaidi  la  Septemba  11, 2001  bila  ya   watuhumiwa  hao  kufikishwa mahakamani. Kwa  mara  ya  kwanza  waziri  wa  sasa  wa  ulinzi na  ambaye  ataendelea  kuwa  waziri  katika  wizara hiyo  Robert Gates amesema  wazi  bila  ya  kusita. Nataka  kulifunga  gereza  la  Guantanamo, na  hii itakuwa  haraka   iwezekanavyo. Robert  Gates  ameyasema  hayo  katika  mahojiano na  televisheni  ya  Marekani  ya  PBS. Katika  wakati huu  inaonekana  kuwa   waziri  huyo  wa  ulinzi   ana mawazo  sawa  na  rais  mteule  Obama. Katika  mazungumzo  yao  na  Obama , ametambua kuwa  kufungwa  kwa   gereza  hilo  la  Guantanamo ni  suala  muhimu  lenye  umuhimu  wa  juu  kwa rais  huyo  mteule. Na  pia  kwa  serikali  yote  ya  rais Obama. Itachukua  muda  gani  hadi  kufungwa  kwa  gereza hilo,  swali  hilo  hakuweza  kulitolea  jibu  sahihi waziri  huyo  atakayekuwa  pia  katika  serikali  ya rais  Obama.  Inawezekana  wafungwa  50  kati  ya wafungwa  wapatao  250  ambao  wanashikiliwa katika  gereza  hilo  wataachiliwa  haraka iwezekanavyo,  kwa  kuwa  kwa  muda  wa  miaka kadha  wameonekana  kuwa  hawana  hatia. Lakini hakuna   nchi  inayotaka  kuwachukua  watu  hao. Inabidi  kuendelea  kutafuta  nchi  ambayo  itakuwa tayari  kuwachukua  watu  hao,  amesisitiza  waziri huyo  wa  ulinzi  wa  Marekani.

Ukweli  ni  kwamba , hatujapata  nchi  ambayo itawachukua. Na  hususan  tunataka  kuwa  na uhakika  kuwa  watu  hao  hawatakamatwa  tena  na kuteswa.

Gates  amewataka  maafisa  wake  katika  wizara hiyo  kutoa  pendekezo  jinsi  ya   kulifunga  gereza hilo, kile  kitakachohitajika   ili  kuweza  kulifunga,  na kuwaondoa   wafungwa  kutoka  katika  gereza  hilo, wakati  huo  huo , wakihakikisha   usalama  wa   watu wa  Marekani  kutokana  na  baadhi  ya  wafungwa ambao  ni  hatari.

Obama  ameahidi   kulifunga  gereza  la Guantanamo, ambalo  limekuja  kuwa  alama  ya matumzi  ya  nguvu  katika   kuwafunga  watu , ambapo imesababisha   Marekani  kushutumiwa  kwa  madai ya  utesaji.

Naamini  uwezo  wa  mahakama  za  Marekani pamoja  na  usalama   wa   jela  zake.

Hayo  amekuwa  akiyasisitiza  kila  mara  Obama wakati  wa  kampeni  za  uchaguzi. 

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22