December 24, 2008

MASHOGA WAKASIRIKA.

Makundi ya mashoga yamekasirishwa baada ya baba mtakatifu Benedikt wa 16 kusema kwamba binadamu anahitaji kukombolewa ili aondokane na mkanganyiko wa jinsia ambao ni hatari.
Akiwahutubia watumishi wa ngazi za juu katika kanisa huko Vatican, Baba Mtakatifu Benedicto wa 16 alisema kuwa kumwepusha mwanadamu na ushoga ni muhimu na kufananisha kuwa ni sawa na kulinda mazingira, kauli ambayo imewakasirisha wanaharakati wa ushoga.
Chama cha mashoga nchini Uingereza LGCM kimesema kuwa kauli ya baba mtakatifu siyo ya kuwajibika na wala haikubaliki.

No comments: