December 23, 2008

UJERUMANI KUPOKEA WAFUNGWA WA GUANTANAMO


Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameelezea kuunga kwake mkono kwa wafungwa wa zamani katika jela la Guantanamo kuletwa Ujerumani.
Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung la hapa Ujerumani limemnukuu Waziri huyo wa Nje wa Ujerumani akisema kuwa mipango ya Rais mteule wa Marekani Barack Obama ya kulifunga gereza hilo la Guantanamo Bay isipate kikwazo cha kukosekana kwa nchi itakayowachukua wafungwa hao.
Kwa upande mwengine serikali ya Ujerumani imesema kuwa inaangalia uwezekano wa kuwachukua watuhumiwa hao.Msemaji wa Wizara ya Nje ya Ujerumani amesema kuwa wizara hiyo imeombwa kuangali kwa kina masuala kadhaa.
Miongoni mwa masuala hayo ni kwa watuhumiwa ambao wanatoka katika nchi zenye mizozo na zisizo na sheria, au ambao hawaruhusiwa kurejea makwao au ambao hawataki kureja kwao.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa muda mrefu amekuwa akiunga mkono kufungwa kwa jela hilo la Guantanamo.
Kwa sasa kuna kiasi cha watuhumiwa wa ugaidi kutoka nchi mbalimbali wapatao 250 ambao wamewekwa katika gereza hilo toka kutokea kwa shambulizi la kigaidi nchini Marekani la September 11.

1 comment:

Anonymous said...

wee! kama huna cha kuongea funga hii blog usituzingue1