January 22, 2009

OBAMA NA GUANTANAMO


Ni siku ya pili tangu kuanza kazi yake ikulu ya White House, kama rais wa Marekani. Na tayari Rais Barack Obama amekuwa na shughuli nyingi tangu kuapishwa kwake siku ya Jumanne.
Lakini suala ambalo limezua hisia kote ulimwenguni ni ile hatua iiliyotarajiwa ya kuitia saini hii leo amri ya kulifunga gereza la Guantanamo.
Nitalifunga gezera la Guantanamo ni kiwa Rais, na kweli ahadi hiyo sasa imetimia pale Rais Barack Obama hii leo kutia saini amri ya kulifunga gereza hilo hii, ambalo limekuwa kero kwa wengi duniani tangu lifunguliwe mwaka wa 2002. Tangu atoe tangazo la kusimamishwa kwa muda wa siku 120 kwa mashtaka yote ya watuhumiwa wanaozuiliwa katika gereza hilo,na hatimaye kutiwa saini kwa amri hiyo hivi leo, maswali mengi yameibuka kuhusu nini hatima ya watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakizuiliwa kwa miaka kadhaa bila kufikishwa mahakani.
Rais Obama anaelekea kutimiza moja wapo ya ahadi alizozitoa wakati wa kampeini, ambapo miongoni mwa yaliyomo kwenye amri hiyo, ni kufanyiwa marekebisho utaratibu wa idara ya ujasusi wa kuwazuia na kuwahoji watuhumiwa na hivyo kuekewa mipaka utaratibu wa kuhojiwa katika magereza yote yanayosimamiwa na Marekani kote ulimwenguni,mbali ya maeneo ya kijeshi. Jengine ni kjuzuiwa kwa shirika ujasusi kuwazuwia kwa siri wafungwa wa ugaidi katika jela za nchi nyengine.

Lakini sasa maswali yanayoibuka ni wapi watakako pelekwa watuhumiwa hao?
Bado kuna jumla ya wafungwa 245 wanaozuliwa katika gereza hilo huku wengi wakiwa wamehukumiwa bila ya kupata nafasi ya kujitetea.
Sara Mendeleson ni mtaalam katika kutio cha mikakati na masuala ya kimataifa mjini Washington. Sara Mendelson anasema..``katika mfumo wa sheria ya uhalifu nchini Marekani, tangu mwaka wa 2001 kuna jumla ya watu 145 waliohukumiwa katika kesi za ugaidi wa kimataifa. Ingawa hakuna ushahidi lakini taarifa zilizokusanywa kuwemo utesaji wa watuhumiwa katika mfumo wa sheria. Hivyo basi panahitajika kamati mpya za waendesha mashtaka na maafisa wa upelelezi wa FBI kufanya uchunguzi na kukusanya ushahidi mpya´´.
Swali ni je baada ya uchunguzi kufanywa watuhumiwa hawa watarudishwa katika nchi waliko, au kufunguliwa mashtaka nchini marekani?.
Baadhi ya mataifa yamejitolea kuwapa hifadhi ya ukimbizi watuhumiwa lakini waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates anasema itakuwa vigumu kwa Marekani.
Robert Gates anasema..``kwangu mimi nahisi tunahitaji sheria mpya ili mtu anapoachiliwa kutoka gereza la Guantanamo asiweze kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini Marekani´´.
China imesisitiza kuwa wafungwa wote wa kichina katika gereza hilo wanapaswa kurudishwa nyumbani ili wafunguliwe mashtaka. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje Jiang Yu alisema kuwa baadhi yao walikuwa wafuasi wa kundi la kigaidi ambalo liko katika orodha ya baraza la usalama la umoja wa mataifa ya yale makundi ya kigaidi ulimwenguni.
Hata hivyo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa muda wa mwaka mmoja uliotangazwa na Rais Obama wa kulifunga Gereza hilo ni mrefu mno, ikizingatiwa mateso walioyapata watuhumiwa hao.

No comments: