February 04, 2009

BARRICK GOLD

Mfuko wa pensheni wa Taifa waondoa hisa zake Barrick Gold ya Canada, inayomiliki migodi ya Bulyanhulu

Mfuko wa pensheni wa taifa wa Norway "The Norwegian Public Service Pension Fund/Statens pensjonskasse", umeondoa hisa zake zote toka kwenye kampuni kubwa ya migodi duniani, Barrick Gold baada ya kashfa kadhaa zinazozihusu Barrick Gold. Moja ya kashfa kubwa ni ya mauaji ya wakazi kadhaa wa Bulyanhulu yaliyofanyika miaka kadhaa iliyopita na serikali ya Tanzania kukataa kufanya uchunguzi wa mauaji hayo, pamoja na mauaji hayo kumekuwa na migogoro kadhaa baina ya wakazi wa maeneo ya karibu na migodi hiyo na wamiliki wa migodi hiyo. Barrick Gold inamiliki migodi.
Sababu nyingine ya kujitoa mfuko wa pensheni ni uchafuzi wa mazingira kwenye makampuni ya migodi inayomilikiwa na Barrick Gold, nchini Papua New Guinea.
Kujitoa kwa mfuko wa pensheni wa taifa wa Norway toka Barrick Gold ni pigo kwa kampuni hiyo na wachunguzi wa mambo wanahisi mfano wa Norway unaweza kuigwa na nchi zingine, hususani za Skandinavia.
Chanzo cha habari: Norwegian TV 2
Zaidi kuhusu Barrick Gold kwenye vyombo vya habari:
http://www.dominionpaper.ca/articles/2385
http://www.corpwatch.org/article.php?id=15265
http://intercontinentalcry.org/uprising-against-barrick-gold-in-tanzania/
http://www.norwatch.no/20080408558/oljefondet/gruveindustri/barrick-gold-i-enda-en-verstinggruve.html
http://vcr.csrwire.com/node/12629
http://www.africafiles.org/article.asp?ID=19871
http://www.radiomundoreal.fm/rmr/?q=en/node/26891
http://gregornot.wordpress.com/2009/01/06/uprising-against-barrick-gold-in-tanzania/
http://www.corpwatch.org/article.php?id=15263
http://www.minesandcommunities.org/article.php?a=8263

Posted by Chama Cha Watanzania Oslo - CCW Oslo

No comments: