February 18, 2009

THELUJI YAIGANDISHA UK

Bila shaka mmiliki wa baiskeli hii alilazimika kutafuta njia nyingine ya usafiri....ilikuwa tabu.
Barabara za masafa marefu zilikuwa ni misururu mirefu ya magari ya kila aina.

Theluji ililazimu kufungwa kwa njia zote mbili za kuruka na kutua ndege kwenye uwanja wa Heathrow.
Huduma ya usafiri wa mabasi ya jiji la London ilisimamishwa kuepusha ajali kutokana na barabara kuwa hazipitiki kwa urahisi
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika makazi ya Waziri mkuu wa Uingereza, Downing Street, jijini London.Wafanyakazi walilazimika kufanya kazi usiku kucha kuondoa theluji.
Theluji nzito ambayo imekuwa ikimwagika katika maeneo mbali mbali ya Uingereza imesababisha kuvurugika kwa huduma za usafiri kwa kiasi kikubwaImeelezwa kuwa kiasi cha theluji iliyoanguka hakijawahi kutokea kwa kipindi cha miaka 18 iliyopita

No comments: