February 19, 2009

WENYE MIKOPO KUNUSURIKA

Thamani ya nyumba Marekani imeshuka na idadi ya watu wanaoshindwa kulipa rehani mwezi baada ya mwezi inaongezeka na kuzua hofu ya wengi kupoteza nyumba zao
Lakini Rais Obama ameahidi kushughulikia tatizo hilo vilivyo, na kuwapa mamilioni ya watu matumaini ya hali kuimarika.
Takriban watu milioni tano wanaomiliki nyumba wataungwa mkono kuendelea kumudu malipo ya mikopo yao ya nyumba.
Mpango huu unanuia kuongeza imani kwa kampuni mbili kubwa zinazotoa mikopo ya nyumba nchini marekani, Fannie Mae na Freddie Mac.
Utawala wa Obama utatoa kiasi kingine cha dola bilioni mia mbili kutoka kwa serikali ili kuwawezesha mamilioni ya Wamarekani kuendelea kumiliki nyumba zao na kuimarisha uchumi ambao unazorota.

No comments: