February 19, 2009

BARUA YA HAMAS KWA OBAMA

Seneta mashuhuri wa Marekani John Kerry anafanya ziara katika ukanda wa Gaza , hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa afisa wa ngazi za juu kutoka Marekani kuzuru Gaza tangu kundi la Hamas lilipochukua udhibiti wa eneo hilo karibu miaka miwili iliyopita.
Bwana Kerry Anatarajiwa kufanya mazungumzo na mashirika ya kimataifa , ikiwa ni pamoja na shirika la umoja wa mataifa la kutoa misaada katika eneo hilo, ambalo vifaa vyake afisi zake ziliharibiwa kwenye mashambulizi ya hivi karibuni .
Bwana Kerry amesema ziara yake haiashirii mabadiliko ya msimamo wa Marekani wa kuepuka kukutana na kundi la Hamas , ambalo Marekani inalichukulia kuwa kundi la kigaidi.
'' Uongozi wenu wa kisiasa unatakiwa kuelewa kwamba taifa lolote ambalo raia wake wanashambuliwa kwa roketi lazima lijibize. Hakuna mabadiliko , hebu niliweke wazi hilo , hakuna mabadiliko kuhusu msimamo huo '', alisema Bwana Kerry.
Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la kupeleka misaada Gaza Karen Abu Zayd amesema kundi la Hamas limetumana barua kwa John Kerry ipelekewe rais Barak Obama
.

No comments: