March 19, 2009

KIFUNGO CHA MAISHA JELA

Josef Fritzl amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa yote yaliyomkabili.
Mtu alietenda uhayawani wa kuzaa watoto saba na binti yake, Josef Fritzl leo amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa yote yaliyokuwa yanamkabili.
Hapo awali kabla ya mahakama ya nchini Austria kutoa adhabu, mtu huyo mwenye umri wa miaka 73 aliomba radhi kwa moyo wake wote kwa kumfungia ndani binti yake na kumbaka kwa muda wa miaka 24
Josef Fritzl mwananchi wa Austria alikiri makosa yake yote ikiwa pamoja na kutembea na kuzaa na binti yake Elisabeth,kumbaka ,kumfungia ndani,na pia amekiri kumuua mtoto mchanga kutokana na uzembe.Mtoto huyo alikuwa mmoja kati ya saba ambao Fritzl amezaa na binti yake. Mdema huyo alikufa kwa sababu ya kukosa matibabu alipokuwa mgonjwa.Juu ya kifo cha mtoto huyo mchanga, Fritzl alipatikana na hatia ya kumuua kutokana na uzembe.
Mahakama ya St.Pölten imemhukumu Josef Fritzl kifungo cha maisha atakachotumikia katika kitengo cha watu wenye matatizo ya akili.Mshitakiwa aliikubali hukumu hiyo, inayoanza mara moja.
Mahakimu wanane walikubaliana kwa kauli moja juu ya hatia ya mauaji ya mtoto mchanga.Kosa hilo pekee limebeba adhabu ya kifungo cha maisha jela.Mtoto huyo alikufa mnamo mwaka 1996 muda mfupi tu baada ya kuzaliwa.
Josef Fritzl aliiambia mahakama kuwa anajuta kwa moyo wake wote juu ya alichokifanya kwa familia yake.Lakini amesema anasikitika kwamba hakuna anachoweza kufanya kusahihisha hayo.Amesema amebakia kutazama tu na kutafuta uwezekano wa kupunguza madhara.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22