May 08, 2009

DENI LA SERIKALI KUFIKIA EURO BILLIONI 80

Waziri wa Fedha wa Ujerumani Peer Steinbrück amesema, deni la serikali mwaka huu litafikia kiwango kipya na kupindukia Euro bilioni 80 kwa sababu ya mzozo wa uchumi na fedha wa hivi sasa. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kutaja tarakimu kinaganaga.
Mpaka sasa, Berlin ilikuwa ikisema kuwa deni jipya litafikia kama Euro bilioni 37. Waziri Steinbrück amesema, kodi ya mapato haitoshushwa katika juhudi ya kufufua uchumi. Vile vile, kodi ya mapato haitaongezwa mpaka mwaka 2013, licha ya kuongezeka kwa nakisi ya bajeti ya serikali.

No comments: