Baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu ,mtuhumiwa uhalifu enzi za utawala wa Manazi "Iwan the Terrible" -John Demjanjuk, Marekani ilimkabidhi leo Ujerumani.Katika gereza karibu na Munich,mzee huyo mwenye umri wa miaka 89 amepangiwa kusomewa waranti wa kutiwa nguvuni.
Sobibor -Poland iliokaliwa na Ujerumani, ndiko ilipokuwa kambi ya manazi ya kuwahilikisha mayahudi.Hadi binadamu 2000 wakiuliwa kila siku katika vyumba vya gesi.Kwa jumla, inakisiwa mayahudi 250.000 walihilikishwa humo.
Walinzi wa kambi hiyo wakiwapakia wahanga wao ndani ya magari-moshi hadi kwenye vyumba hivyo vya gesi.Halafu wakiwazika maiti katika makaburi ya umma wa watu na baadae wakisafisha vyumba hivyo vya gesi tayari kwa kundi jengine.
Mmoja kati ya walinzi hao waliosaidia kuwahilikisha mayahudi hao atuhumiwa kuwa mzaliwa wa Ukraine .John Demjanjuk.Yasemekana baina ya mwezi machi na septemba, 1943 alishiriki katika kuwahilikisha hadi mayahudi 29,000.Alitimiza kazi hiyo akisaidiwa na wasaidizi wa kujitolea waliofunzwa kazi hiyo katika kambi ya mafunzo ya Manazi.Hii ni kwa mujibu wa nyaraka zinavyoonyesha.
Kwamba Demjanjuk alikuwa mateka na mfungwa wa Ujerumani ya Manazi na alijitolea kufanya kazi hiyo kwa kuhofia maisha yake ,hali hiyo haipunguzi hatia yake.Hata hivyo, Demjanjuk anakanusha tuhuma hizo zote na anasema, hakujua kile kilichokua kikipita katika kambi ya Sobibor na baadae ile ya Majdanek na Flossenburg.Binafsi, anadai alikuwa mfungwa wa vita.Lakini kwa jicho la ushahidi uliopo na kutokana na ujuzi wa kihistoria ,madai yake hayaaminiki sana.Kwani, Demjanjuk alikuwa mzungushaji gurudumu la kiwanda cha mauaji....
Kwa kesi yake mjini Munich ,inaanza mojawapo ya kesi za mwisho za Manazi nchini Ujerumani.Ni kesi dhidi ya mzee aliefikisha sasa umri wa miaka 89 na pengine mgonjwa. ...
Demjanjuk anapewa mashtaka ya kisheria ambayo yanazingatia umri na afya yake .Bila ya shaka, kesi yake itakuwa ngumu,itakayozorota muda mrefu na matokeo yake hayajulikani.Taabu itakuwa kumtwika pekee mabegani mwake jukumu la yaliopita na ushahidi wake. Kwahivyo, je, kesi hii haifai kuendeshwa ? La, hasha.
Iwapo Demjanjuk ataishia gerezani Ujerumani ni jambo linalotiliwa shaka shaka kubwa.Mahakama za Ujerumani baada ya kupita zaidi ya miongo 6 tangu kumalizika utawala wa vitisho wa manazi, zinaweka wazi kuwa, hakuna yeyote aliyeusaidia utawala wa manazi kuhilikisha wenzake au aliyeutumikia,afaa leo kusamehewa.Umri pekee hautoshi kukwepa hatia. Kesi mjini munich pia ni dalili ya kusikizwa malalamiko dhidi ya unyama na ushenzi uliopita.
muhimu zaidi ni ishara inayokwenda kwa wale walionusurika kuhilikishwa na kwa jamaa zao, Kesi hii ni kutumikia ukweli,haki na utu bila kutegemea iwapo mwishoe, Demjanjuk atapitishiwa adhabu yoyote....
No comments:
Post a Comment