

Akielezea Blog ya jamii mratibu wa mashindano hayo Nashe Mvungi amesema wasanii wa muziki wa kizazi kipya MB Dogg na Bushoke watapanda jukwaani kutumbuiza, mbali na hao kutakua na makundi mengine ya burudani kutoka sehemu mbalimbali za Ulaya.
Katika kinyangányiro hicho mgeni wa heshima ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mheshimiwa A.Ngemera.
Akizungumzia washiriki wa mashindano hayo Nashe alisema nafasi bado ziko wazi kwa watakaotaka kushiriki, form za kushiriki zipatikana katika www.misstanzania.eu au email info@misstanzania.eu
Vile vile mratibu huyo alisisitiza kuwa washindi wa 3 wa mwanzo watapata nafasi ya kwenda United Kingdom kwenye mpambano wa Miss Tanzania mjini London.
No comments:
Post a Comment