May 01, 2009

Ulimwengu waadhimisha siku ya wafanyikazi.

 

Waadamanaji 39 wakamatwa,na polisi 30 kujeruhiwa walipokuwa wakiyazuia maandamano ya wafanyikazi mjini Berlin nchini Ujerumani.

 

Leo ulimwengu mzima unaadhimisha siku ya wafanyakazi na mjini Berlin hapa Ujerumani, waandamanaji 39 wamekamatwa na polisi 30 kujeruhiwa walipokuwa wakiyazuia maandamano ya wafanyakazi. Makabiliano mengine kama hayo kati ya polisi na waandamanaji yametokea mjini Hamburg hapa ujerumani. Kwingineko nchini Taiwan karibu wanachama elfu 10 wa vyama vya wafanyakazi wameandamana wakilaani serikali kwa kutochukua hatua zozote kukabiliana na upungufu wa ajira.

Katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin polisi elfu tano zaidi wanashika doria kuzuia machafuko yoyote ya waandamanaji wa mrengo wa kushoto, ambao wamekuwa wakifanya maandamano haya siku hii ya mei mosi kwa miongo miwili, ili kutoa kero zao.

Maafisa wa Ujerumani wanataraji idadi ya waandamanaji kuongezeka mwaka huu kutokana na nchi hii kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi tangu vita vya pili vya dunia. Waandamanaji hao walishambulia treni na  magari kwa chupa na mawe huku wakisababisha uharibifu katika vituo vya mabasi kwa kuvunja vyoo.

Nchini Ufaransa vyama vinane vikuu vya wafanyikazi vimeitisha maandamano ya kitaifa, kulalamikia jinsi rais Nicholas Sarkozy anavyoushughulikia uchumi, hii ikiwa ni mara ya tatu kwa vyama hivyo kuitisha maandamano kama hayo mwaka huu. Maandamano mengine ya vyama vya wafanyakazi pia yanatarajiwa mjini Madrid nchini Uhispania.  

Maelfu ya wanachama wa vyama vya wafanyikazi, walioandamana leo mjini Taipei nchini Taiwan.Maelfu ya wanachama wa vyama vya wafanyikazi, walioandamana leo mjini Taipei nchini Taiwan.

Barani Asia hali si tofauti, kwani karibu wanachama elfu 10 wa vyama vya wafanyikazi nchini Taiwan wameendamana leo mjini Taipei kulalamikia  hatua ya serikali kuzuia  kukabiliana na upungufu wa ajira kisiwani humo. Mmoja wa waandalizi wa maandamano hayo, amesema hali nchini humo imeendelea kuwa mbaya zaidi lakini serikali haijachukua hatua zozote kuimarisha uchumi na kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa kazi.

Karibu waandamaji 100 baada ya maandamano hayo walijaribu  kuingia kwa nguvu katika ofisi za mawaziri ili kumwona waziri mkuu Liu Chao-Shiun, kueleza kutoridhishwa kwao kutokana na kile wanachodai ni hatua ya serikali kutojishughulisha  kuongeza nafasi za kazi nchini Taiwan

Hata hivyo walizuiwa na polisi kuingia katika ofisi hizo. Kutokana na mgogoro wa masoko duniani, uchumi wa Taiwan ulipungua kwa zaidi ya asilimia 8 katika robo ya mwisho ya mwaka jana, na serikali inatabiri huenda ukapungua kwa  zaidi ya asilimia 2.7 mwaka huu. Kwa jumla karibu wataiwan millioni 1.37  wanaotegemewa na familia zao wamepoteza ajira.

Nchini Uturuki polisi katika mji mkuu Istanbul wamekabiliana na mamia ya waandamanji na kulazimika kutumia maji kuwatawanya na baadhi yao kutiwa mbaroni.

Kwa mujibu wa mwandishi mmoja wa  blog hii aliyekuwa katika eneo la tukio,waandamaji hao waliokuwa katika wilaya ya Sisli waliwarushia polisi mawe.

Bunge la Uturuki Jumatano wiki hii walipitisha kuwa sheria kuwa mei mosi ni  sikukuu ya kitaifa baada ya kuondolewa katika orodha ya sikukuu nchini humo kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1980.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22