May 16, 2009

Pato la ndani lashuka kwa asilimia 3.8 nchini Ujerumani

Katika robo ya  kwanza ya mwaka huu pato la ndani  lilinywea  kwa  asilimia 3.8  nchini  Ujerumani.

Idara kuu ya takwimu imetoa taarifa hiyo leo mjini  Berlin  inayoonesha kwamba Ujerumani ,hakika imo katika kina kirefu  cha  mdodoro  wa uchumi kisichokuwa na kifani tokea kumalizika vita kuu  ya  pili.Uchumi wa Ujerumani ulirudi nyuma katika robo ya kwanza  ya mwaka huu.

Idara kuu ya takwimu ya serikali ya mjini Wiesbaden imearifu  kwamba pato la ndani ya nchi lilinywea kwa asilimia  3.8   katika kipindi hicho.Wataalamu  wa uchumi wamesema Ujerumani haijawahi kukabiliwa  na mserereko  wa uchumi wa  kiwango hicho  tokea kumalizika vita kuu vya pili.

Hii ni kwa mara ya nne mfululizo kwamba  pato la taifa limenywea  nchini Ujerumani. Kupungua kwa pato la taifa kunafuatia kunywea  kwa uchumi  wa nchi kwa  asilimia 2.2  katika robo ya mwisho ya mwaka  jana.Wataalamu  wa  uchumi wamesema hawakutarajia mserereko huo mkubwa.

 Hata hivyo uchumi wa Ujerumani ulionyesha dalili za kuanza  kutengemaa mnamo mwezi wa aprili.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22