May 17, 2009

UCHUMI WA TANZANIA LEO

Mh.Balozi A.R. Ngemera akiwa na wafanyabiashara wa kijerumani waliyowekeza nchini Tanzania katika sekta ya utalii kupitia kampuni yao  Manyara Valley Culture Camp.Wa mwisho kulia ni  mkufunzi wa chuo kikuu cha Tumaini Iringa, Eli Laitika ambaye anasoma mjini Munich. 

Mh Ngemera akioneshwa picha za mradi wa kampuni hiyo ya Manyara Valley Culture Camp katika kongamano hilo. www.4tanzania.com
Baadhi ya watanzania waliyoudhuria kongamano hilo kutoka kushoto,Eli mkufunzi wa chuo kikuu cha Tumaini  Iringa,Malumbo Salim mdau mkuu wa Munich na Augsburg,Eric Moro mdau wa Nuremberg,Aboubakary Liongo wa Deutsche Welle na Luteni Ben Kitego anayekula kitabu mjini Munich. 

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh Ahmada Ngemera amewahakikishia wafanyabiashara wa Ujerumani wanaotaka kuwekeza Tanzania, kuwa mazingira ya kuwekeza nchini humo ni mazuri na ya kuvutia.

Alisema hayo katika kongamano la uchumi  ambalo liliandaliwa na chama cha urafiki wa watanzania na wajerumani na kuudhuriwa na wafanyabiashara na wawekezaji wa kijerumani kutoka katika jimbo la Munich ambalo ndiyo tajiri kabisa nchini Ujerumani.

Balozi Ngemera amesema pamoja na kuyumba kwa uchumi wa dunia, lakini bado uchumi na mazingira ya tanzania ni ya kuvutia kwa wawekezaji kwa nia ya kuwekeza.

Aidha alisema serikali imedhamiria kwa dhati kupambana na rushwa ambayo ilianza kupigwa vita toka enzi zu mwalimu Nyerere.

Hata hivyo alikiri kuwa kasi ya kuchukua hatua si kubwa kama ilivyo katika nchi zu Ulaya, akitolea mfano wa kashfa ya rushwa iliyolikumba kampuni moja kubwa la magari la hapa Ujerumani, ambapo serikali ilichukua hatua zu haraka.

Lakini Balozi Ngemera amesema, serikali inajitahidi kuongeza kasi hiyo ya kupambana na ufisadi.

Pia alizungumzia suala la ardhi ambapo alisema ni suala nyeti lakini lisiwatishe wawekezaji kwani tanzania ina Sera mujarab katika suala zima la ardhi.

Hata hivyo alisema haiwezekani muwekezaji akapewa ardhi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula, lakini yeye akatumia kwa kilimo cha mazao mfano ya kutoa mafuta.
 
Akizungumzia juu ya mchango wa sekta ya wafanyabishara wadogo wadogo hususan wanawake, Balozi Ngemera alisema wawekezaji katika lengo hilo wanakaribishwa ambao watavisaidia vikundi vya kinamama.

Wakati huo huo Balozi huyo wa Tanzania nchini Ujerumani ameanza utaratibu maalum wa kuwatembelea na kukutana na watanzania wanaoishi katika majimbo ya hapa Ujerumani.

Ujerumani ni moja kati ya nchi kubwa Barani Ulaya ambapo imekuwa vigumu kwa watanzania kukusanyika sehemu moja kutoka sehemu mbalimbali.

Watanzania kadhaa wametoa pongezi kwa hatua hiyo ya BALOZI Ngemera ya kuwa karibu na watanzania na kusema anatekeleza kivitendo tabia ya Rais Jakaya Kikwete ambaye anasifika kwa kuwa karibu na wananchi wa chini.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22