June 12, 2009

Gaddafi azungumza dhidi ya Marekani katika hotuba yake katika baraza la seneti

Kiongozi wa Libya anayeitembelea Itali Mohammar Gaddafi ameifananisha Marekani na kundi la kigaidi la al-Qaeda na kuishutumu kwa kuiruhusu Iraq kuwa taifa la Kiislamu lenye msimamo mkali katika hotuba kali jana Alhamisi kwa maseneta wa Italia.
Akikumbushia shambulio la mabomu katika mwaka 1986 dhidi ya Libya ambalo liliua watu kadha ikiwa ni pamoja na mtoto wake alihoji iwapo kuna tofauti kati ya mashambulio ya Marekani dhidi ya Libya na hatua za kigaidi za al-Qaeda.
Gaddafi ambaye alipata mapokezi makubwa wakati wa kuwasili kwake mjini Rome siku ya Jumatano amesema kuwa dunia inaishi katika kivuli cha ugaidi rasmi, na kwamba Osama bin Laden hana taifa lakini Marekani ni taifa.
Amesema kuwa Libya inapinga ugaidi , na kuongeza kuwa haitoshi kushutumu ugaidi, lakini ni muhimu kuangalia chanzo cha ugaidi.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22