Italia imeridhia kuwachukua wafungwa watatu waliokuwa wakizuiliwa katika jela la Guantanamo iliyoko Cuba.Kauli hizo zimetolewa baada ya Rais Barack Obama wa Marekani kukutana mjini Washington na Waziri Mkuu wa Italia
Rais Obama aliahidi kulifunga jela hilo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na amekuwa katika harakati za kuzishawishi serikali nyingine za bara la Ulaya kuridhia kuwahifadhi baadhi ya wafungwa wanaoaminika kuwa hawana hatari yoyote tena.Jela la Guantanamo lilifunguliwa punde baada ya mashambulio ya mabomu yaliyotokea Washington na New york mwezi Septemba mwaka 2001.
Tangazo hilo la Italia limetolewa baada ya Marekani na Umoja wa Ulaya kuafikiana hapo jana kuwa na mpango maalum utakaoyawezesha mataifa wanachama ya umoja huo kuwapokea baadhi ya wafungwa wa Guantanamo.Kulingana na Rais Obama kauli za serikali ya Italia zinaonyesha kuwa nchi hiyo inaunga mkono harakati zake za kulifunga jela la Guantanamo.Rais Obama alifafanua kuwa hatua hiyo itawapa fursa ya kutunga sheria mwafaka za kimataifa zitakazopambana na ugaidi jambo litakalowanufaisha wahusika wote alisema ''Itakapohitajika chini ya misingi ya sheria na usalama wa kitaifa tutajaribu kuwahamishia baadhi ya wafungwa katika magereza maalum yanayotumiwa kuwazuia wahalifu hatari kote nchini.Tunapochukua uamuzi huu kumbukeni ya kwamba hakuna mtu hata mmoja aliyefanikiwa kutoroka kwenye magereza ya nchi hii yaliyo na ulinzi mkali.
No comments:
Post a Comment