Takwimu zilizotolewa na Umoja wa Ulaya zimeonesha kuwa kiasi cha watu millioni 1.2 kwenye nchi zinazotumia sarafu ya Euro katika umoja huo wamepoteza ajira zao katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu.
Kiwango hicho ni mara mbili ya idadi ya watu waliyopoteza ajira zao katika kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka 2008.
Wataalam wa uchumi wanasema kuwa hali hiyo imesababishwa na kuendelea kuparaganyika kwa uchumi na kushuka kwa biashara kunakohatarisha faida yote hayo yakiwa ni kutokana na mgogoro wa kiuchumi duniani.
No comments:
Post a Comment