Hali ni tete Somalia. Kundi la wapiganaji wa al Shabab wametisha kuwashambulia wanajeshi wowote wa kigeni watakaoingia Somalia ili kuisaidia serikali kupambana na uasi. Uongozi wa nchi hiyo umeyatolea wito mataifa jirani Kauli hizo zinazoungwa mkono na Umoja wa Afrika. Wakati huo huo, katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu, OIC, ameitolea wito jamii ya kimataifa kuingilia kati. Kiasi cha watu 300 wameuawa katika mapigano hayo yaliyodumu kwa kipindi cha majuma sita yaliyopita. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa mataifa, wengine 125,000 wameachwa bila makazi.
Kundi la al Shabaab limeonya jana kuwa endapo vikosi vya vya kigeni vitaingia Somalia kuisaidia serikali wapiganaji hao watakuwa hawana budi kuwashambulia. Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa kundi la al Shabaab, Sheikh Ali Mohammed Rage, aliyefanya mkutano na waandishi wa habari mjini Mogadishu.
Kauli hizo zimetolewa baada ya spika wa Bunge la Somalia, Sheikh Aden Mohamed Nur Madobe, kuyatolea wito mataifa jirani ya Djibouti, Kenya na Ethiopia kuvipeleka vikosi vyao katika kipindi cha saa 24 kwa minajili ya kuisaidia kupambana na uasi.
No comments:
Post a Comment