June 12, 2009

Wachina wanne waislamu waliokuwa Guantanamo wapelekwa Bermuda

Kisiwa cha Bermuda kinachomilikiwa na Uingereza kimewapokea raia wanne wa China waislamu au Uighurs kama wanavyofahamika,waliokuwa katika jela ya Guantanamo Cuba.Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari,wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imekasirishwa na hatua hiyo kwa kile walichokitaja kuwa haijashauriwa kikamilifu kuhusiana na suala hilo.Hatua hiyo pia imeikasirisha serikali ya mjini Beijing ambayo hapo jana ilisisitiza kwamba wafungwa wote 17 raia wake wanaoshikiliwa katika jela hiyo warudishwe nyumbani.China bado inawatazama wafungwa hao wa zamani kama ni magaidi licha ya Marekani kuwaondolea tuhuma za kuwa kitisho kwa usalama wa taifa.Mpaka sasa ni wafungwa sita kati ya kiasi 240 katika jela hiyo walioachiliwa tangu mwezi wa januari.Hii imetokana na matatizo ya kupatikana nchi zinazoweza kuwakubali watu hao.Rais Barack Obama wa Marekani ameahidi kuifunga jela hiyo kufikia mwanzoni mwa mwaka ujao.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22