July 24, 2009

Mkuu wa kampuni ya Porsche ajiuzulu

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni kubwa la kutengeneza magari ya kifahari hapa Ujerumani ya Porsche,Wendelin Wiedeking, amejiuzulu nafasi yake hiyo mnamo wakati ambapo kampuni hiyo ikijaribu kukabiliana na hali ngumu ya fedha inayoikabili.

Bodi ya usimamizi ya kampuni hiyo ya Porsche katika kikao chake cha usiku kucha jana, mbali ya kurudhia hatua hiyo ya kujiuzulu kwa Wiedeking, pia imetangaza kuidhinisha kiasi cha Euro billioni 5 katika mtaji wa kampuni hiyo.

Wiedeking, ambaye imekuwa ikielezewa kuwa ni kati ya wakuu wa mashirika waliyokuwa wakilipwa mshahara mkubwa nchini Ujerumani, atalipwa kiinua mgongo cha kiasi cha euro millioni 50, nusu ya hicho lakini kitakwenda katika mfuko wa jamii.

Hatua hiyo pia inafungua njia kwa shughuli za kampuni hiyo kuchukuliwa na kampuni lingine kubwa la magari la Volkswagen. Pia bodi hiyo iliridhia ombi la muwekezaji kutoka Qatar ambaye anataka kununua hisa katika kampuni hiyo.

No comments: