August 24, 2009

Jinsi kampuni ya Opel inavyoweza kuathiri pirika pirika za uchaguzi nchini Ujerumani

Kizungumkuti cha kampuni ya magari la Opel,kampeni za uchaguzi mkuu na kumalizika mashindano ya kimataifa ya riadha mjini Berlin ndizo mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.
Tuanze na kisa cha kampuni ya magari ya Opel inayokumbwa na kitisho cha kufilisika.Gazeti la "Bild"-Zeitung la mjini Berlin linaandika:
Katika kadhia ya Opel serikali kuu ilitaka kwa kila hali kuepusha kampuni hiyo ya magari isijitangaze muflis.Makampuni mawili tuu,ile ya Canada,Magna na benki ya Urusi-Sbrebank ndio yaliyokua yakipewa nafasi nzuri ya kuiokoa kampuni hiyo ya Opel .Pendekezo la kampuni ya wawekezaji ya Ubeligiji - RHJ lilipuuzwa.Hivi sasa serikali kuu ya mjini Berlin inakumbwa na kizungumkuti.Kampuni mama ya-General Motors haina pupa na wala haishughulishwi na uchaguzi mkuu utakaoitishwa hivi karibuni nchini Ujerumani.Hata serikali ya Marekani haivutiwi na fikra ya kuiona benki ya serikali ya Urusi ikidhamini hatima ya tawi la Opel mjini Rüsselsheim.Yote hayo yanaweza kuwapatia shida waokozi wa Opel,Merkel na Steinmeier.Kwakua serikali kuu ya muungano inatakiwa ijibu kwa kila hali kabla ya september 27 ijayo General Motors inaweza hadi wakati hupo kupandisha bei itakavyo.Na kwa namna hiyo uhusiano pia pamoja na rais mpya wa Marekani unaweza kufujika bila ya kutaka.Kwa vyovyote vile kadhia ya Opel ni linatupatia funzo la kisiasa linalobainisha kwamba serikali si wajasiri mali bora.
Tunaingia katika kampeni za uchaguzi mkuu ambazo zimepamba moto humu nchini.Gazeti la " Abendzeitung" la mjini Munich linaandika:
"Tukitilia maanani maoni ya umma na ya wadadisi wa kisiasa,basi matokeo ya uchaguzi yanajulikana hata kabla ya wananchi kuteremka vituoni.Baada ya september 27,maoni hayo yanaashiria kuingia madarakani mjini Berlin serikali ya muungano wa rangi nyeusi na manjano .Lakini serikali kama hiyo inataka nini hasa?Kuna wanaoamini kweli kwamba katika enzi hizi za shida, kansela Angela Merkel na mwenye kujipendekeza kwa wananchi Seehofer wataweza kweli kukubaliana kutia njiani mageuzi ya kina kuhusu kodi za mapato? Serikali ya muungano ya Nyeusi na Manjano ikiingia madarakani basi itakua tuu kwasababu wananchi wamechoshwa na serikali ya muungano wa vyama vikuu na hawaiangalii kwa jicho jema serikali ya muungano ya vyama vya mrengo wa shoto vya rangi nyekundu-nyekundu na kijani.

Mji mkuu wa Ujerumani sio tuu umejitembeza ipasavyo,lakini hata wageni wake wameridhika na jinsi maandalizi ya mashindano hayo yalivyokua.Wanariadha kutoka kila pembe ya dunia wamefurahia na kushukuria jinsi mashabiki walivyowapa moyo bila ya kupendelea walipokua wakitimka katika uwanja wa Olympik mjini Berlin.Na wanariadha wa Ujerumani nao jee?Na kwao wao pia ,mashindano haya ya kimataifa yamefana.Sio tuu kwamba picha za televisheni zimeonyeshwa katika zaidi ya nchi 190,bali nchini pia watu wamejionea mashindano hayo.Kati ya watazamaji milioni sita na milioni 10 waliangalia kwa siku mashindano hayo

No comments: