September 07, 2009

KAMPENI ZA UCHAGUZI UJERUMANI

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wa chama cha kihafidhina CDU ameanzisha awamu ya mwisho ya kampeni ya uchaguzi utakaofanywa Septemba 27. Amesema, ni lazima kwa CDU/CSU

kuchomoza imara katika uchaguzi ujaoChama cha Kansela Merkel CDU kimekuwa madarakani pamoja na chama cha kisoshalisti SPD kwa miaka minne iliyopita lakini sasa, Merkel anataka kujitoa kutoka muungano huo na badala yake kushirikiana na waliberali wa FDP wanaoelemea zaidi upande wa wafanya biashara. Katika hotuba yake mbele ya kiasi ya wanachama 9,000 mjini Düsseldorf, Merkel alisifu mafanikio ya serikali ya muungano wa vyama vya vikuu CDU/CSU na SPD tangu mwaka 2005. Amesema Ujerumani imesonga mbele hasa katika sekta ya elimu, utafiti, sera za familia na imeweza kuongeza nafasi za ajira. Kwa mfano, katika tangu serikali hiyo ya muungano kushika madaraka mwaka 2005,kiasi ya watu milioni moja wamepata ajira na wanatoa mchango wao katika bima ya huduma za jamii. Lakini sasa wakati umewadia kwa Ujerumani kuwa na mageuzi.Kuna haja ya kuwa na serikali ya kihafidhina itakayoongozwa na vyama ndugu vya CDU/CSU na waliberali FDP.Amesema suala ni iwapo Ujerumani ifuate mrengo wa wastani kwa utulivu na tahadhari au itumbukie katika hali isiyo wazi kisiasa. Uchaguzi wa Septemba 27 unahusika na suala hilo.Akaongezea:

" Tunataka muamue kwa neema ya taifa na hiyo itawezekana ikiwa tu CDU na CSU vitakuwa na nguvu."

Uchunguzi wa mwisho wa maoni umeonyesha kuwa CDU na CSU vinaweza kujikingia asilimia 35 hadi 37 ya kura katika uchaguzi wa Septemba 27 na FDP kati ya asilimia 14 na 15. Chama cha SPD kinajikokota kwa asilimia 23. Licha ya CDU kupata pigo kubwa katika chaguzi za Agosti 30 katika majimbo matatu, chama hicho katika daraja ya taifa kinaendelea kungwa mkono.

Merkel binafsi hakumshambulia waziri wa mambo ya nje Frank-Walter Steinmeier wa SPD anaegombea ukansela vile vile, lakini wanachama waandamizi wa CDU wameeleza shaka zao kuhusu msimamo wa Steinmeier katika suala la kuundwa serikali ya muungano pamoja na vyama vya mrengo wa kushoto Die Linke. Baadhi ya wanachama wa CDU wanahisi kuwa Steinmeier huenda akashirikiana na chama cha Kijani na Die Linke kuunda serikali, ikiwa CDU na FDP havitopata wingi wa kutosha katika uchaguzi wa Septemba 27. Kampeni ya uchaguzi huo ikiendelea kushika kasi, Merkel na Steinmeier wanatazamiwa kushiriki katika mdahalo wa televisheni Septemba 13..


No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22