Ushindi huo utamuwezesha Bibi Merkel kuunda serikali na chama cha Kiliberali cha FDP.Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa na kituo cha televisheni cha ZDF chama cha CDU/CSU kimepata asilimia 33.5 ya kura zote na FDP kimepata asilimia 14.5
Kwa pamoja kura za vyama hivyo viwili vimevipiku vyama vingine vitatu
vikubwa vilivyosalia.Kutokana na hali hiyo Bibi Merkel ataweza kuvunjilia mbali muungano wa CDU na SPD uliokuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mine iliyopita.Ushirikiano wao na chama cha Kiliberali cha FDP kinachounga mkono masuala ya biashara utamuwezesha Bibi Merkel kuyapa msukumo zaidi masuala ya kupunguza kodi pamoja na kuuongeza muda wa kuvitumia viwanda vya nuklia.Chama cha Kisoshalisti cha SPD kimeripotiwa kupata asilimia 23.5 takwimu zinazoaminika kuwa za chini zaidi tangu kukamilika kwa vita vikuu vya dunia.Chama cha Kijani GrĂ¼ne kimepata asilimia 10 nacho cha mrengo wa shoto Die Linke nacho kimejikusanyia asilimia 13.
Bibi Merkel anapendwa
Tofauti na hali ilivyokuwa Marekani na Japan wapigaji kura wa Ujerumani hawakuonekana kutaka mabadiliko ya uongozi uliokuwapo.Wengi wanaripotiwa kuwa na imani na mfumo wa Bibi Merkel ambaye ni Kansela wa kwanza wa kike wa Ujerumani na ni mgombea pekee wa ngazi hiyo anayetokea eneo la Mashariki lililokuwa likisimamiwa na utawala wa Kikomunisti.
Uchaguzi huu unafanyika wakati muhimu ambapo Ujerumani iliyo na uchumi wa tatu kwa ukubwa barani Ulaya inajikwamua kufuatia mtikisiko wa kiuchumi uliougubika ulimwengu kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Serikali mpya italazimika kupambana na bajeti inayokabiliwa na madeni,uhaba mkubwa wa kazi pamoja na athari zilizosababishwa na mparaganyiko wa kiuchumi jambo ambalo litayafanya mabenki kuvipunguza viwango vyao mikopo inayotoa.
No comments:
Post a Comment