September 16, 2009

MTANZANIA ATUHUMIWA KUMUUA MWANAWE

Mbongo mmoja aliyejulikana kwa jina la la Ibrahim Kibayasi,amearestiwa kwa Obama (USA) akituhumiwa kumuua mwanawe mwenye umri wa miezi 5.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti jana, Mbongo huyo atapandishwa kwa pilato wakati wowote kujibu mashitaka ya mauaji.

Mtoto huyo aliyeuawawa..alifariki dunia Jumatano iliyopita baada ya kulazwa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni dalili za ugonjwa unaotokana na kupigwa.

“Tuhuma za mauaji zilitarajiwa kufunguliwa Ijumaa (juzi) dhidi ya baba wa mtoto wa miezi mitano ambaye alifariki dunia Jumatano baada ya kulazwa hospitali, kwa kile kilichoelezwa na mamlaka kuwa ni kutokana na dalili za ugonjwa unaotokana na kupigwa,” alisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mamlaka za Marekani zimesema,Kibayasi ni raia wa Tanzania,alikwenda nchini humo miaka saba iliyopita kwa viza ya mwanafunzi, na ilishakwisha muda wake.

Habari zaidi zinasema, Mtanzania huyo anayeishi Block 1700, Barabara ya Sable alidhaminiwa kwa dola za Marekani milioni mbili sawa na zaidi ya Sh bilioni mbili za Tanzania.

Waendesha mashtaka wa Serikali ya Marekani wamesema wanajiandaa kufungua mashitaka mapya ya mauaji na wanatarajia kutoa masharti mengine ya dhamana.

Polisi wa Mt. Prospect walimkamata Kibayasi Septemba 3 mwaka huu baada ya watumishi wa hospitali ya Advocate Lutheran iliyoko Park Ridge kuwataarifu kuwa mtoto huyo wa kiume alionekana kama amepigwa.

Pia idara ya Huduma kwa Watoto na Familia ya Illinois ilitoa taarifa polisi kwamba maumivu ya mtoto huyo yanaonekana kuwa yametokana na kupigwa.

Waendesha mashitaka walidai kuwa siku ya tukio la kupigwa kwa mtoto huyo, Kibayasi alikuwa amebaki na mtoto huyo nyumbani wakati mama yake akiwa kazini.

Inadaiwa kwamba mtoto huyo alimkasirisha kijana huyo,akambeba na kumtikisa kwa nguvu mara kadhaa huku akimtupa kitandani.

Kwa mujibu wa madai hayo, baadaye Kibayasi alimbeba mtoto wake huyo na kumfuata mama wa mtoto huyo kazini. Mama huyo alipoona hali ya mtoto huyo alipiga simu ya polisi kuomba msaada.

Kwa mujibu wa habari hizo, mtoto huyo alipofikishwa hospitalini wahudumu wa hospitali walimchukua na kumweka katika chumba cha wagonjwa mahututi akawa anapumua kwa msaada wa mashine.

Aidha habari hizo zilidai kwamba madaktari waliokuwa wakimtibu mtoto huyo waligundua majeraha katika mbavu yaliyokuwa yameanza kupona.

Katika taarifa iliyohifadhiwa kwenye mkanda wa video, Kibayasi anadaiwa alikiri polisi kuwa wiki chache zilizopita alimshika na kumminya kwa nguvu mtoto huyo sehemu za kiunoni.

Waendesha mashitaka wanadai kuwa pamoja na kumuumiza mtoto huyo hakumpeleka hospitali.


No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22