September 17, 2009

Ras Nas ziarani Norway, 2009

Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya rege na muziki wa dansi mwenye makao yake Oslo, Norway, Ras Nas aka Nasibu Mwanukuzi, kwa hivi sasa anapanga safu kali kwa ajili ya ziara ya miji sita Norway. Ziara hiyo itakayoanza Kongsberg tarehe 23 Oktoba itamalizikia jijini Trondheim 7 Desemba. Kikosi cha Ras Nas kinachanganya wanamuziki toka Congo Brazzaville, Ivory Coast, Norway na USA. Wabongo wa Norway habari ndiyo hiyo!


Mwezi wa Desemba Ras Nas na bendi yake watatembelea miji ya Galle na Colombo Sri Lanka kuwasilisha Norway, (ofkozi na Tizedi vile vile) katika tamasha la muziki. Kwa habari zaidi fuatilia
http://www.rasnas.kongoi.com.

Asanteni kwa kusoma habari hii.

Kongoi Productions

http://www.kongoi.com

No comments: