Rais Barack Obama wa Marekani leo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobeli kwa mwaka huu wa 2009.
Rais Obama ameshinda tuzo hiyo ikiwa si zaidi ya mwaka tokea aingie madarakani na amewashinda zaidi ya watu 200 waliopendekezwa kuwania tuzo hiyo.
Akizungumza wakati wa kutangaza tuzo hiyo Mwenyekiti wa kamati ya Nobeli Thordjorn Jagland amesema kamati hiyo imezingatia juhudi za kipekee za Rais Barack Obama katika kuimarisha diplomasia ya kimataifa.
Mshindi wa mwaka jana wa tuzo hiyo Rais wa Finland Martii Ahti-saari ambaye alishinda kutokana na juhudi zake za upatanishi amesema kuchaguliwa huko kwa Obama ni kumtia moyo kuendelea na masuala hayo.
Tuzo hiyo yenye thamani ya dola milioni 1.4 anatarajiwa kukabidhiwa rasmi rais Obama Desemba 10 mjini Oslo-Norway
No comments:
Post a Comment