January 12, 2010

Timu ya Togo yarejea nyumbani


Timu ya taifa ya kandanda ya Togo imerejea nyumbani, kutoka Angola ilikojitoa katika michuano ya Afrika kufuatia shambulio dhidi yao lililofanywa na waasi katika mji wa Cabinda.

Timu hiyo imerejea ikiwa na miili ya kocha msaidizi na afisa habari wa michezo ambao pamoja dereva wa basi lao waliuawa katika shambulio hilo hapo siku ya Ijumaa.

Waziri Mkuu wa Togo Gilbert Fossoun Houngbo alitangaza kujitoa kwa nchi hiyo ingawaje wachezaji walitaka kuendelea na mashindano.

Naye Waziri wa michezo wa Togo Christophe Tchao akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kupanda ndege iliyotumwa na serikali yao, alisema kuwa ameliomba shirikisho la soka barani Afrika CAF kuangalia uwezekano wa kuiweka tena nchi hiyo katika ratiba ya michuano hiyo baada ya siku tatu za maombolezi.

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22