July 27, 2010

FFU wa Ngoma Africa kuvamia Frankfurt City
Ngoma Africa Band kukiwasha cha moto ! Afrika-Karibik Festival, Frankfurt
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "The Ngoma Africa Band" aka FFU
wanatarajiwa kutua kwa nguvu zote !katika onyesho kubwa la Afrika & Karibik Festival,
litakalofanyika katika Viwanja vya Robestock Park, Frankfurt,Ujerumani siku ya Jumamosi
07-08-2010 maelfu ya washabiki wa muziki nchini Ujerumani wanaisubiri bendi hiyo kwa hamu kubwa...
kutokana na mdundo wake unaochezeka.
habari zinatonya kuwa bendi hiyo pia itatingisha jukwaa katika onyesho lingine kubwa
la Festival mjini kaiserslautern,Ujerumani siku ya Jumapili 8-08-2010 ambako katika kila
hali washabiki wapo tayari kwenda sambamba na gwaride la FFU wa Ngoma Africa band.
usikose kujipa raha mwenyewe kwa kuwasikiliza hapa www.myspace.com/thengomaafrica

1 comment:

Anonymous said...

kamanda wa ffu ,naomba kuliza swali?hivi kwanini mara nyingi unakuwa umevaa miwani meusi hata usiku? au unawaonea aibu wale unawaimba imba ktk nyimbo zenu?