August 28, 2010

KITUKO CHA MUHINDI

Kuna Muhindi mmoja alienda Katika Super market huko Australia. Katika pita pita ndani ya Super market akaona chakula cha paka cha kwenye makopo. Akachukua akaenda kulipia kaunta.

Manager wa Supermarket akawa na wasiwasi kuwa inawezekana yule Muhindi kaelewa kile ni chakula cha binadamu. Hivyo akamkatalia akamwambia alete paka wake ndo auziwe kile chakula cha paka maana kilikuwa ni sumu kwa binadamu.

Muhindi akaenda hadi nyumbani kwake akamleta paka wake Manager akakubali auziwe kile chakula.

Siku nyingine Muhidi yule yule akaenda kwenye Supermarket ile ile. Katika pita pita akaona chakula cha Mbwa cha kwenye makopo. Akachukua akaenda kulipia kaunta.

Manager wa Supermarket kama kawaida yake akadhani yule Muhindi hafugi Mbwa na kaelewa kuwa kile ni chakula cha binadamu. Basi akamwekea ngumu alete Mbwa wake ajiridhishe anafuga Mbwa ndiyo auziwe.

Muhindi akaenda hadi nyumbani kwake akamleta Mbwa wake, Manager akakubali auziwe kile chakula.

Siku nyingine tena, Muhindi yule yule akaenda kwenye Supermakert ile ile akiwa na begi amening’iniza begani. Kufika tu akamwambia Manager waSupermarket aingize mkono wake ndani ya begi lile.

Manager akaingiza akasikia kitu kilaini laini na chenye unyevu nyevu. Manager akamuuliza Muhindi nini kipo ndani ya begi?

Muhindi akamjibu ‘Sasa naweza nunua Toilet Paper?’


NAWATAKIA WADAU WOTE WEEKEND NA RAMADHANI NJEMA


No comments: