September 02, 2010

Ras Nas kufanya shoo kali Oslo Jumamosi hiiRas Nas aka Nasibu Mwanukuzi na skwadi yake wako tayari kufanya shoo ya kufa mtu kwenye kiota cha maraha jijini Oslo, Skuret Konsertscene, Jumamosi hii. Mambo yataanza saa nne usiku. Sasa wabongo waishio Oslo kazi kwenu, habari ndio hiyo! Wanamuziki wa Ras Nas ni Aris Milongo (Congo), Uriel Seri (Ivory Coast), Chuck Frazier (Texas), Dag Pierre (Sweden) na Thomas Langvann (Norway). Vile vile atakuwepo Dj Dominic (UK) akikwaruza santuri kabla na baada ya shoo.

No comments: