December 22, 2010

Visa zimetolewa kinyume na Sheria katika balozi za Ujerumani

Katika balozi kadha za Ujerumani kuanzia mwaka 2007 kumekuwa kukitolewa visa za kusafiria kinyume na sheria. Taarifa hizo zimetolewa kwanza mwishoni mwa juma na kuthibitishwa siku ya Jumatatu tarehe 20.12. Ubalozi unaozungumziwa sana katika taarifa hii ni wa Misr. Hali hiyo inakumbusha tukio ambapo serikali ya wakati huo ya chana cha SPD na Kijani viliunda tume ya bunge kuchunguza suala hilo.

Msemaji wa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle hakuweza kutambua matamshi yake kuwa hayakubaliani. Kuna baadhi ya matukio yanapita bila kuonekana , anaeleza Andreas Paeschke, kwamba katika utaratibu mkali wa udhibiti katika wizara ya mambo ya kigeni kuna tokea hali kama hiyo. Lakini kutokana na kuwapo karibu maombi milioni mbili ya visa kila mwaka ni wazi kwamba matatizo kama haya yanaweza kutokea ,amesema Paeschke.

Polisi na mwanasheria mkuu wa serikali ya Ujerumani kwa pamoja katika maelezo yao tangu mwaka 2007 wamesema kuna kazi kubwa ya kufanywa, hususan katika kile kinachoshukiwa kuwa ni utaratibu kinyume na sheria wa utoaji wa visa katika ubalozi wa Ujerumani mjini Cairo, lakini pia katika balozi nyingine za kigeni.

Ni suala linalohusu baadhi ya maombi yanayofikia 100 ya visa, ambayo yako katika misingi isiyoeleweka. Katika matukio mengine ni maombi mawili, au matatu. Ni matukio yaliyotokea katika bara la Afrika ama balozi ndogo katika mashariki ya kati, ni katika tukio moja tu ambapo nchi ya Ulaya magharibi inahusika katika eneo la Balkan na jingine limetokea katika Asia ya kati. Katika ripoti za vyombo vya habari kuna nchi pia kama za Amerika ya kusini, lakini hii si kweli.

Wengi wa wafanyakazi wanaofanyakazi katika balozi hizo waliachiliwa huru baada ya kuhojiwa, anaeleza msemaji huyo wa wizara ya mambo ya kigeni.

Wafanyakazi wa balozi, ambao hutoa huduma za kutoa visa , hubadilishwa mara kwa mara katika idara ya visa. Maombi ya visa hutawanywa katika idara mbali mbali bila kuwapo utaratibu maalum. Iwapo kuna shutuma katika mojawapo ya maeneo , mara moja hushughulikiwa suala hilo kwa pamoja na polisi na mwendesha mashtaka. Na kama ni lazima huchukuliwa hatua mara moja.

Matukio ya hivi sasa ya utoaji wa visa kinyume na sheria yanakumbusha matukio kama hayo yaliyotukia mwaka 2004 katika ubalozi wa Ujerumani mjini Kiev. Wakati huo kulikuwa na maelfu ya wasafiri ambao walitiliwa shaka waliopewa visa, ambapo ilikuja kugundulika kuwa ulikuwa mtandao wa watu wanaosafirisha watu uliofaidika na kadhia hiyo, ambapo kulikuwa na wafanyakazi wa biashara ya ngono ambao ni wa kulazimishwa ambao walisafirishwa kuja nchini Ujerumani.

Chanzo:DW-Bonn

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22