August 11, 2011

Sinema Fupi Inaitwa KARMA

Baraka na Frank wa Urbanpulse

URBAN PULSE CREATIVE inawaletea cinema fupi inayoitwa KARMA. Sinema hii fupi ilitengenezwa na Baraka Baraka Kutoka Urban Pulse wakati wa masomo kama assignment ya mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha DE MONTFORT hapa mjini Leicester mwaka 2007 ambapo kila mwanafunzi alitakikana kutengeneza stori yenye kueleweka chini ya dakika Nne bila kutumia maneno bali ni vitendo tu.
Maudhui ya Sinema hii yametokana na misingi ya Dini ya Kihindu yakimaanisha kwamba kila Tendo lifanywalo huwa na madhara yake. Kwa lugha nyingine inamanisha kuwa Ukianzisha balaa, balaa litakurudia hivyo ni vizuri tukawa tunafikiria mara mbili mbili kabla hatujafanya maamuzi magumu.
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE

No comments: