August 29, 2011

Notting Hill Carnival

URBAN PULSE CREATIVE wakishirikiana na Miss Jestina Blog wanakuletea matukio katika picha ya Notting hill Carnival iliyofanyika Jumapili tarehe 28 agosti 2011. Hii ilikuwa siku ya kwanza Carnival ya watoto ambayo hufanyika kila mwaka tangu mwaka 1964 ikifuatiwa kesho yake siku ya jumatatu ikiwa siku ya watu wazima. Maelfu ya watu zaidi walijitokeza katika mitaa ya Notting hill wakati wa Carnival ya jana ambayo ni tofauti na miaka yote pia nyongezo ya polisi 1000 wa ziada na kufanya Jumla ya polisi 6500 kwa ajili ya usalama na kufanikisha shuguli nzima ya wanachi walio hudhuria. Hii inatoka na maasi yaliyo tokea hivi karibuni katika kitongoji cha Tottenham na sehemu nyingine nchini Uingereza. Jumla ya watu 53 wanashikiliwa na polisi kutokana kutaka kufanya fujo jana katika carnival.
Hii ni Carnival kubwa kuliko zote za mabara ya ulaya na ni ya pili kwa dunia
Msanii Kutoka Urban Pulse alifanya makamuzi katika Carnival hii iliyohudhuriwa na watu wengi, mmojawapo wa wadau waliojitokeza kumuunga mkono ni msanii Page kutoka Xfactor.
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE NA MISS JESTINA BLOG

No comments: