August 29, 2011

Futari Mji wa Reading‏


READING EASTERN AFRICAN COMMUNITY(REACO) Iliandaa futari maalum jana jioni 28.8.11 na kuwaalika wanajumuia mbalimbali kutoka Reading, London, Coventry na sehemu nyingine ili kupata futari kwa pamoja. Hii ni desturi ambayo hufanyika kila mwaka wakati huu wa mwezi mtukufu ramadhani. Lengu kuu haswa ni kujumuika pamoja katika kudumisha upendo, amani na umoja kwa wana jumuia pamoja,kuzingatia yale yote yalio mema na kukataza yalio Mabaya.
Mgeni Rasmi wa siku ya leo alikuwa Mh Naibu Balozi Chabaka Kilumanga alieambatana na baadhi ya maofisa wa ubalozi wetu wa Tanzania Hapa London.
Kwa niaba ya Mwenyekiti wa REACO Said Mahmud tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioitikia mwito na kuja kujiunga nasi. Tunawashuru sana.
Kwa maelezo au mawasiliano zaidi tafadhali tutumie email ifuatayo, reaco@hotmail.co.uk
Asanteni,
URBAN PULSE CREATIVE

No comments: