September 12, 2011

RAMBIRAMBI KWA WALIOPATA AJALI YA MELI ZANZIBAR TOKA MONTREAL-CANADA

Ndugu zetu Watanzania,

Kwa niaba ya Watanzania na wananchi wote wa Afrika Mashariki waishio hapa Montreal- Canada, tumezipokea kwa majonzi na mshtuko mkubwa taarifa za ajali ya kuzama kwa meli ya MV Spicer jana usiku, tarehe 10/9/2011 iliyosabababisha vifo vingi vya Watanzania wenzetu kutoka Zanzibar.

Kwa niaba ya Uongozi wa Montreal Tanzanians Association (http://www.montrealtanzanians.com/), tunapenda kutoa salamu zetu za rambirambi kwa wananchi wote wa Zanzibar na Pemba na Tanzania kwa ujumla waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki zao wapendwa katika kindi hiki kigumu cha maombolezo.

Na pia tungependa kuwapa pole wote waliokoka kwenye ajali hiyo ya kusikitisha na tunawaombea kwa M/Mungu awapuguzie maumivu na awape nguvu na faraja.

Mwisho kabisa, Montreal Tanzania Association (MTA) ingependa kutoa shukrani na pongezi za dhati kwa wote walioshiriki katika harakati za kuokoa maisha ya wahanga wa ajali hii na pia katika shughuli za kuopoa maiti.

Tunamuomba Mwenyezimungu aziweke mahali pema peponi nafsi za wote waliopoteza maisha yao kwenye ajali hii. Ameen.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.

Uongozi,

http://www.montrealtanzanians.com/ (MTA)

No comments: