September 13, 2011

SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI

Salam za Rambirambi kutoka kwa Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
Watanzania tunaoishi ujerumani tumesikitishwa sana na habari mbaya ya ajali ya meli iliyotokea 10.09.11 katika bahari ya hindi katikati ya visiwa vya Pemba na Unguja nchini Tanzania. Ajali hii ni pigo na msiba mkubwa kwa Taifa letu. Salam za rambirambi ziwafikie Familia za wafiwa, Viongozi wa Tanzania, na watanzania wote kwa ujumla.

Umoja wa watanzania ujerumani (UTU) kwa masikitiko makubwa tunaungana na wanafamilia, na taifa zima katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa vyombo mbali mbali kwa jitihada zake za kuokoa maisha na kusaidia kwa namna moja au nyingine katika janga hili kubwa kwa Taifa
Tunaomba kwa mwenyezimungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi amen

kny ya UTU

Mfundo Peter Mfundo
Mwenyekiti

No comments:

 Wale wajanja wote tunakutana Leverkusen 24.09.22