September 19, 2011

Wanaume waingia Ubalozini Uingereza‏URBAN PULSE CREATIVE na Miss Jestina Blog wanakuletea Ziara ya Wanaume kutoka kundi la TMK wakiwalishwa na Mh Temba na Chege walipopata fursa ya kutembelea Ubalozi wetu hapa mjini London kabla ya kumaliza show zao hapa nchini Uingereza siku chache zilizopita. Vilevile waliweza kutembelea idara mbalimbali na kujionea jinsi gani Ubalozi wetu hapa London unavyofanya kazi hususani katika idara nyeti ya Uhamiaji inayoongozwa na ofisa Ambokile na Kupiga Picha za pamoja wakiwa na Mh Naibu Balozi Mh Chabaka Kilumanga Pamoja na baadhi ya maofisa wa Ubalozi.

Baada ya Ziara yao Freddy Mtoi Kutoka BBC alifanya nao mahojiano maalum ndani ya ubalozi na yatarushwa hewani duniani kote.

Asanteni,

Ziara hii iliandaliwa na Urban Pulse pamoja na miss Jestina Blog Ikishirikiana na Ubalozi wetu

No comments: