July 24, 2012

KAMBI YA ILALA YAENDELEA KUMFUA BONDIA IBRAHIMU CLASS

Kocha wa Mchezo wa ngumi Kambi ya Ilala Habibu Kinyogoli katikati akiwaelekeza mabondia Yohana Robert KUSHOTO NA Ibrahimu Class jinsi ya kutupa masumbwi kwa mpizani kwa kunyoosha mkono Class anajiandaa na mpambano wake na Simba Watundulu siku ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee jijini Dar es salaamBondia Ibrahimu Class kushoto akipambana na Yohana Robart wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambnano wake na Simba Watundulu utakaofanyika siku ya Idi pili katika ukumbi wa Diamond Jublee.KAMBI ya ngumi Ilala ipo kwenye maandalizi mazito ya kumnoa bondia Ibrahimu Class '
Ibra Mawe' anaetarajia kuzipiga na Simba Watundulu katika uzito wa KG,60 litakalofanyika siku ya Idi pili katika ukuimbi wa Diamond JubleeAkizungumza mmoja wa makocha wa kambi ya ilala inayongozwa na Kocha mkongwe wa mchezo huo Habibu Kinyogoli, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema katika kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani wanamwandaa bondia Ibrahimu Class kwa ajili ya mpambano huo utakaofanyika siku hiyoSuper D alisema wamemuandaa bondia wao kufanya vizuri hili kuweza kumzibiti mpinzani wake kwa kuwa wanamjua uchezaji wake awapo ulingoni hivyo wanamfundisha mbinu mpya kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake. Kambi hiyo ya ngumi imewataka wadau wa mchezo uho kuja kuangali mchezo mzuri wa masumbwi utakaoneshwa na bondia wao kutoka kambi ya ilala.
Ibrahimu Class anaetamba kwa jina la Ibra Mawe yupo chini ya maandalizi makali chini ya makocha wake Kinyogoli na Super D kwa ajili yampambano huo na kuwataka wapinzani wake kwa sasa wakae chonjo kwa kuwa moto umesha washwa na akuna wa kuuzima kwa bondia huyo chipkizi na mwenye nia ya kuupaisha mchezo wa masumbwi Kimataifa mabondia hawo watakuwa wakicheza katika mpambano wa utangulizi wa raundi 6 uku pambano kuu ni kati ya Ramadhani Shauli wa Tanzania na Sande Kizito wa Uganda watakaopambana kugombania mkanda wa Ubingwa wa IBF Afrika.
Source. Super D

No comments: