KATIBU MKUU WA UN BAN KI MOON
Urusi na China kwa pamoja zimelipigia kura ya veto azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililotaka kutumika kwa Ibara ya Saba ya Mkataba wa Umoja huo kuichukulia hatua kali Syria na kusitisha umwagaji damu.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, na msuluhishi wa kimataifa, Kofi Annan, wamezitaka nchi wanachanma wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutatuwa mkwamo wao juu ya na namna ya kukomesha umwagaji damu nchini Syria ambapo washirika wa kijeshi watatu wa karibu wa Rais Bashar al Assad waliuwawa hapo jana.
Makundi mawili ya waasi nchini Syria ambazo zinasema Assad amekuwa akipoteza udhibiti wake kwa mji wa Damascus na kuzidiwa nguvu na upinzani yamedai kuhusika na mripuko huo wa bomu uliotokea ndani ya makao makuu za usalama mjini Damascus.
Annan ambaye anataka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kulipigia kura azimio lilnalungwa mkono na mataifa ya Magharibi ambalo linapingwa na Urusi amesema nchi hizo wanachama lazima ziungane kuwa kitu kimoja kuchukuwa hatua muhimu ili kwamba Syria iingie katika mazungumzo ya suluhisho wa kisiasa.
Azimio la Uingereza linagusia Ibara ya Saba ya mkataba wa Umoja wa Mataifa ambapo Urusi inadai kwamba hatimae linaweza kuepelekea kutumika kwa hatua za kijeshi kama vile ilivyokuwa kwa mashambulizi za Jumuiya ya Kujihami ya NATO huko Libya.
Serikali ya Syria imemteua Fahad Jassim al- Freij kuwa Waziri wa Ulinzi kufuatia kifo cha Daoud Rajha. Wakati huo huo, machafuko yanazidi kuripotiwa katika maeneo ya mji mkuu, Damascus.
Wanaharakati wanaoupinga utawala wa Syria wanasema vikosi vya serikali vimeendelea kuyashambulia maeneo ya mjini mkuu Damascus, siku moja baada ya mashambulizi ya bomu kuua watu wa karibu wa Rais Bashar -al -Assad. Wakati huo huo, Assad yuko katika mji wa bandari ya Latakia, akiongoza operesheni ya jeshi lake na taarifa zinadai kuwa atakuwepo hapo kwa siku kadhaa.
Kwa mujibu wa maelezo ya wanaharakati wa upinzani mjini Damascus, askari wanaomtii Rais Bashar al- Assad wamevishambulia viunga vya mji mkuu huo leo na kuzidisha hali ya hofu kwa wakaazi wake.
Ghasia zimeripuka asubuhi ya leo jirani kabisa na makao makuu ya serikali baada ya waasi kupambana na vikosi vya serikali, ambavyo vimeeneza magari yao ya kivita na kuongeza vizuizi vya barabarani katika maeneo ya mji mkuu.
Shirika la haki za binadamu la Syria lenye makao yake makuu Uingereza limeripoti kuwepo kwa machafuko maeneo mbalimbali nchini Syria ukiwemo mji wa Ikhlas ambapo mtu mmoja ameuwawa. Mauaji hayo yametokea mkabala na jengo kubwa la baraza la mawaziri na kampasi ya Chuo Kikuu cha Damascus.
Raia waukimbia mji mkuu Damascus
Wakazi wa mji wa Mezzeh wameonekana wakiukimbia mji huo kuokoa maisha yao, baada ya vikosi hivyo kuuzingira na kushambuliana na waasi wa eneo hilo.
Assad yuko katika msiba wa shemeji yake pamoja na Daoud Rajha, Waziri wa Ulinzi, Assef Shawkat (shemeji mtu) na Jenerali Hassan Turkmani viongozi wawili wa juu wa jeshi. Mpaka sasa haijulikani iwapo Assad alikuwa mjini Latakia wakati wa kuuwawa kwa vigogo hao watatu au la
Mkoa wa Latakia uliopo mwambaoni mwa Bahari ya Mediteranian ni makaazi ya wafuasi wa madhehebu ya Alawite, ambayo yanamjumuisha Assad.
Tayari Fahad Jassim al- Freij amekwishateuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi wa Syria.
Marekani na Uingereza zasemaje?
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Leon Panetta amesema "Hii ni hali ambayo inazidi kukithiri kwa uharaka sana. Na kwa sababu hiyo, ni muhimu mno kwamba Jumuiya ya Kimataifa, kushirikiana na mataifa mengine yanayohusika katika eneo hilo, ili kuleta mbinyo mkubwa kwa Assad."
Na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema sasa ni muda wa Rais Assad kuondoka madarakani.
No comments:
Post a Comment