July 20, 2012

Kenya na Ethiopia kupambana katika Olimpiki

Huku mashindano ya Olimpiki yakinukia nukia, kenya na Ethiopia zinatarajiwa kuendelea kudhihirisha umahiri wao wa kitamaduni kama nchi zenye nguvu zaidi za bara afrika kutafuta medali katika mashindano hayo.
Huku Afrika Kusini ikishindwa kuwafikia wanariadha wa kike na kiume kutoka Afrika Mashariki katika mbio, ina matumaini ya kuimarika baada ya matokeo duni katika mashindano ya Olimpiki mjini Beijing miaka minne iliyopita wakati wanariadha wake 253
Nigeria ni nchi nyingine ambayo ni lazima iamimi kuwa unaweza kufanya vyema na kupata medali zaidi katika mashindano hayo.
Timu nyingine za Afrika zimejizatiti vilivyo kujaribu kupata nafasi katika vitengo mbalimbali katika kivumbi hicho cha Julai 27 hadi Agosti 12, na timu za Afrika Kusini za mchezo wa magongo za wanawake na wanaume pamoja na timu ya mpira wa kikapu ya Angola zimeonyesha hamu kubwa ya kufanya vyema.
Kenya ndiyo ilikuwa bora miongoni mwa mataifa ya AFRIKA katika mashindano ya Beijing kwa kunyakua medali sita za dhahabu, nne za fedha na nne za shaba, ikiwa ni jumla ya medali 14, idadi iliyoongezeka mara mbili kutoka kwa ile waliyopata katika mashindano ya Olimpiki ya Athens mwaka wa 2004.
Nafasi ya tatu waliyoipata katika mashindano ya riadha ya Daegu Korea Kusini mnamo mwaka wa 2011 inaonyesha kuwa Wakenya ni wapinzani wa kimataifa. Huku kifo cha utata cha bingwa wa mbio za marathon Samuel Wanjiru kikiweka wingu jeusi, wanariadha Wilson Kipsang, Abel Kirui na Emmanuel Mutai walichaguliwa kuiwakilisha kenya na wanaonekana kuwa warithi tosha wa Wanjiru.
Kikosi cha Kenya cha wanariadha wa kike katika mbio za Marathon kinawajumuisha Mary Keitany, Edna Kiplagat na Priscah Jeptoo kimeangazia macho yao kwa medali ya dhahabu, baada ya nishani za fedha za mwaka wa 2004 na 2008 alizoshinda Catherine Ndereba. Aidha matumaini yako juu kwa mwanariadha Vivian Cheruyiot katika mbio za mita 5,000 na 10,000.
David Rudisha ni miongoni mwa wanaopigiwa upatu katika mbio za mita 800, lakini huenda akapata ushindani mkali kutoka kwa mwanariadha anayeimarika kwa kasi wa Ethiopia mwenye umri wa miaka 18 Mohamed Aman. Miongoni mwa magwiji wa mbio za masafa marefu wa Ethiopia ni Haile Gebrselassie aliyeshindwa kufuzu kwa mashindano ya London, lakini anaamini anawakabithi mwenge wanariadha wa kizazi chipukizi wakiongozwa na Kenenisa Bekele.
Baada ya kuduwazwa na mwenzake Yonah Blake mara mbili katika kipindi cha siku tatu, mwanariadha wa kasi zaidi ulimwenguni ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki Usain Bolt amejiondoa katika mashindano ya riadha ya Diamond Legaue mkondo wa Monacho yatakayofanywa mwishoni mwa mwezi huu.
Kocha wa Bolt, Glen Mills amesema baada ya Bolt kushiriki katika majaribio ya kitaifa ya kukichagua kikosi cha Jamaica katika mashindano ya Olimpiki mjini Kingston, mwishoni mwa wiki ambako alikuwa na matatizo kidodo, amemwondoa katika mbio za Monaco ili kumpa muda wa matibabu na kufanya mazoezi.
Bolt atatetea mataji yake ya mbio za mita 100, 200 na mia moja wanariadha wanne kupokezana vijiti katika mashindano ya Olimpiki mjini London kuanzia tarehe 27 Julai.

No comments: