April 15, 2013

MASHOGA AFRIKA KUSINI WAFUNGA NDOA YA KWANZA YA KIMILA BARANI AFRIKA



Tshepo Cameron Modisane (kushoto) na Thoba Calvin Sithole (kulia), wakivishana pete wakati wa ndoa yao ya kimila ya mashoga ambayo inadhaniwa kuwa ya kwanza kufungwa nchini humo kwa mujibu wa mtandao wa Huffington.
Tshepo Cameron Modisane na Thoba Calvin Sithol, wanaume wawili raia wa Afrika Kusini, wameripotiwa kufunga ndoa katika mji wa KwaDukuza katika Jimbo la KwaZulu-Natal, mbele ya wageni 200 katika hafla ambayo iliwajumuisha watu wa mila za makabila ya Wazulu na Watswana.
Wanandoa hao wote wakiwa na umri wa miaka 27 watafunga ndoa nyingine ya kawaida na ya kisasa jijini Johannesburg baadaye mwaka huu kwa mujibu wa habari zilizopatikana.
"Hatua tuliyoifanya tukiwa mashoga ni kujitambulisha kwa familia zetu,” Tshepo aliliambia shirika la mtandao lijulikanalo kama Mamba Online mwezi Feburari.
Aliongeza kwamba: “Tumebarikiwa kuwa na familia zinazotuunga mkono. Japokuwa sisi ni mashoga, lakini bado ndugu zetu wanatupenda.”
Wanaume hao wanatumaini kupata watoto kwa kupitia watu wengine.
“Familia ni jambo muhimu kwetu, ndiyo maana tunataka kuwa na watoto,” alisema Thoba na kuongeza kwamba, “tunataka watoto wetu wakue katika mazingira ambayo watapendwa na wazazi wa pande zote.”
Mwaka 2011, gazeti la GlobalPost liliielezea Afrika Kusini kuwa “sehemu bora zaidi -- na sehemu mbaya zaidi – kwa kuendesha ushoga” ambapo lilielezea pia kuenea kwa vitendo vya ubakaji dhidi ya wanawake wanaoendesha vitendo vya ngono baina yao mbali na vitendo vya udhalimu wa kingono unaoendeshwa dhidi ya wanawake na watoto.

Source:Teentz

No comments: