August 14, 2013

Walter Chilambo Afunguka Baada ya Kuchanwa na Ney Kuwa Ana Maisha Duni Licha Ya Kushinda Milioni 50 za EBSS

Baada ya maneno na tuhuma nzito za Ney wa Mitego dhidi ya Mshindi wa Epiq Bongo Star Search mwaka 2012, Walter Chilambo kuwa 'huenda' amedhulumiwa zawadi yake ya ushindi, Shilingi Milioni 50 na waratibu wa shindano hilo kwa sababu mpaka sasa yupo katika maisha duni, Msanii huyu amevunja ukimya na kusema kuwa yeye yupo vizuri tu.
Walter amesema kuwa maneno haya hayana ukweli wowote na yeye anaishi vizuri tu na kwa Ney, Hadhani kama alikaa chini na kufikiria kabla ya kuongea kuhusiana na issue hii katika wimbo wake, wala hakufanya uchunguzi wowote ambao uliomhusisha yeye.
Walter amesema kuwa yeye na Ney hawana ukaribu wowote, na walishawahi kukutana hivi karibuni na alipomuuliza ni kwanini amemuimba vile katika wimbo wake, Ney alimwambia kuwa 'asipanik' then akapotezea na mambo issue nyingine na kisha kutimua zake.
Walter amemaliza kwa kusema kuwa, Maneno haya hayamuumizi vile hayana ukweli wowote, na vilevile hayawezi kumuondolea mashabiki wake.

Source:Teamtz

No comments: