August 11, 2013

WASANII WENGI WA FILAMU TANZANIA WALALAMIKA MIKATABA MIBOVU


Batulli  ambaye  ni mmoja wa waigizaji wa kike warembo anayekuja kwa kasi  nchini na ambaye jina lake halisi ni Yobnesh  a.k.a Nesh, amefunguka kwenye Twitter kuwa licha ya soko la movie kupanuka, waigizaji wengi hawana kitu.
“Wasanii wengi wa filamu huwa tunaamka asubuhi hata hatujui tutakula nini. Accounts zetu hazina kitu wakati tuna film nyingi sana sokoni,” ametweet.
“Wenzetu huamka na mipango kamili ya siku iliyopo lakini wasanii wa film huwa tunaamka huku tukiwaza ni nani wa kumpiga kibomu siku ipite.
"Jina kubwa umejibana umepata gari yako 1 tena used, siku ukiipeleka garage unashinda na wewe huko huko garage kazi zote unasimamisha #Huruma.”
Batulli ameilalamikia pia mikataba mibovu iliyopo kwenye filamu.
“Mikataba ya kazi za film Tanzania ukiisoma unaweza ukajuta kwanini uliamua kuwa muigizaji, unauza movie yako na haki miliki kwa miaka 50.
"Hakuna anaependa ndio maana tunalia na serikali mikataba ibadilishwe tupewe kipaumbele movie niuze leo nimiliki baada ya 50 yrs? 

1 comment:

Mkala said...

Inasikitisha jinsi wasanii wanvyobanwa, 50 years later movie hiyo haitokuwa na thamani yeyote na atarithi mjukuu wako labda, ukifanikiwa kuzaa na mwanao akazaa pia. Umefikia wakati wasanii na waongoza filamu wawe na umoja wa kweli na ili wafanikiwe kuna kujitoa mhanga kama kulala njaa, kukosa pesa ya kufanyia service ya gari na kadhalika, sioni kuwa kuna wasanii wenye uwezo wa kujitolea kiasi hicho kama ilivyo kwa wale wa Bongo flava!